Advertisement |
TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI - WATENDAJI WA VIJIJI (NAFASI 37)
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda anapenda kuwatangazia Wananchi wote wenye sifa kutuma maombi ya nafasi ya kazi ya Watendaji wa Vijiji Daraja la III kwa kuzingatia Maelekezo na Vigezo vilivyoainishwa hapa chini:
SIFA:
- Awe amehitimu kidato cha IV au VI, amehitimu mafunzo ya Astashahada / Cheti (Technician Certificate) kati ya fani zifuatazo: Utawala, Sheria, Elimu ya Jamii, Usimamizi wa Fedha, Maendeleo ya Jamii na Sayansi ya Sanaa kutoka chuo chochote kinachotambuliwa na Serikali.
- Awe ni Mtanzania mwenye umri kati ya miaka 18 hadi 45
- Awe tayari kufanya kazi katika Vijiji vilivyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.
KAZI ZA KUFANYA / MAJUKUMU:
- Atakuwa Mtendaji na Mshauri mkuu wa Serikali ya Kijiji Kamati zake katika mipango ya maendeleo
- Atakuwa Afisa Masuuli na Mtendaji Mkuu wa Serikali ya Kijiji
- Atakuwa Mhasibu wa Serikali ya Kijiji na atasimamia Mapato na Matumizi ya Serikali ya Kijiji
- Atakuwa Mlinzi wa Amani na msimamizi wa Utawala bora katika Kijiji
- Atatafsiri Sera, Utaratibu na kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogo ndogo za Halmashauri katika Kijiji
- Atakuwa Katibu wa Kamati ya Halmashauri ya Kijiji
- Ataongoza vikao vya maendeleo ya Kijiji vitakavyowahusisha wananchi na wataalamu waliopo kwenye eneo lake
- Atatekeleza majukumu yote kadri atakavyokuwa anaelekezwa na Mwajiri wake
NGAZI YA MSHAHARA:
Mshahara ni kwa mujibu wa viwango vya mshahara Serikalini yaani TGS B (390,000/=) kwa Mwezi.
MASHARTI MENGINE:
- Maombi yote yaambatanishwe na maelezo binafsi yanayojitosheleza (detailed CV)
- Barua za maombi ziambatane na Picha 2 (Passport size) za hivi karibuni na ziandikwe majina kwa nyuma
- Barua ya maombi iwekwe namba ya simu inayopatikana wakati wote
JINSI YA KUOMBA:
Maombi yote yatumwe kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya S.L.P 126, Bunda na yaambatane na nakala ya vyeti kama ilivyoelekezwa hapo juu.
Mwisho wa kupokea maombi ni Tarehe 08/04/2018 saa 9.30 alasiri
Limetolewa na Mkurugenzi Mtendaji (W),
S.L.P 126,
BUNDA
0 comments: