Friday, 23 March 2018

Nafasi 33 za Kazi ya Mtendaji III Halmashuri ya Wilaya ya Kishapu, Mwisho wa Kutuma Maombi ni Tarehe 30 March 2018

ad300
Advertisement


Nafasi 33 za Kazi ya Mtendaji III Halmashuri ya Wilaya ya Kishapu 

Kumb No. KDC.P.70/2/VOL II/131 

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Kishapu anapenda kuwatangazia Watanzania wenye sifa za komba nfasi za kazi ya Watendaji wa Vijiji kwa marharti ya kudumu, tangazo hili ni baada ya kupokea kibali cha ajira mbadala chenye kumbu Na. CFC 26/2015/01 "F"/91 cha tarehe 22/08/2017 pamoja na barua ya nyongeza ya muda wa utekelezaji wa kibali cha ajira mbadala kwa watendaji wa Vijiji na mitaa chenye Kumb Na, CFC.26/205/01/"GG"/95 cha tarehe 12/03/2018 vyote kutoka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora 

mchanganuo wa fani ni kama ifuatavyo 

1. MTENDAJI WA VIJIJI III NAFASI 33 

i. SIFA ZA MWOMBAJI
- awe amehitimu elimu ya kidato cha 4 na 6 
- waliopata mafunzo ya stad katika ngazi ya cheti (NTA level 5) ambayo amehitimu kutoka chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo Dodoma au chuo kingine chochote kinachotambulika na Serikali 

ii MSHAHARA
kwa kuzingatia ngazi ya mishahara ya serikali yaani TGB 

iii. KAZI NA MAJUKUMU
- afisa masuuli na mtendaji mkuu wa Serikali ya Kijiji
- Kusimamia ulinzi na usalama wa raia na mali zao kuwa malinzi wa amani na msimamizi wa utawala bora katika kijiji
- kuratibu na kusimamia upangaji wa utekelezaji wa mipnago ya maendeleo ya kijiji
- katibu wa mikutano yna kamati zote za halmashauri ya Kijiji
- kutafsiri na kusimamia sera, sheria na taratibu
- kuandaa taaarifa za utekelezaji wa kazi katika eneo lake na kuhamasisha wananchi katika kuandaa na kutekeleza mikakati ya kuondoo njaa, umaskini na na kuongeza uzalishaji mali
- kiongozi Mkuu wa Vitengo vya kitaalamu katika kijiji
- Kusimamia, kukusanya na kuhifadhi kumbukumbu zote na nayaraka za kijiji
- kupokea na kusikiiza na kutataua malalamiko na migogoro ya wnanachi
- kusimamia utungaji wa sheria ndogo za kijiji
- atawajibika kwa Mtendaji kata 

MASHARTI YA JUMLA
i. mwombaji lazima awe raia wa Tanzania 
ii. awe na miaka 18 - 45
III. Waombaji wenye vyeti vya kughushi usijaribu kumba nafasi hizi endapo utabainika hatua za kisheria zitachukuliwa
iv. awe hajawahi kufukuzwa kazi, kupunguzwa, kuachisha au kustaafishwa kazi katika utumishi wa Umma
v. awe tayari kufanya kazi katika kijiji chochote cha kishapu
vi. waombaji waambatanishe vivuli vya vyeti vya shule, taaluma kuzaliwa na vitambulisho vya taifa kwa wale waliondikishwa
viii. CV tarifa binafsi ya mwombaji
ix. mwombaji aambatanishe na picha ndogo 2 za hivi karibuni
x. siku ya usaili kila mwombaji afike na vyeti vyake halisi vya shule na taaluma pamoja na kuzaliwa 
xi. mwombaji aadike kwa usahihi anuani yake na namba ya simu iayopatikana muda wote kwaajili ya mawasiliano
xii. mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 30/03/2018
xiii. maombi yaandikwe kwa mkono bla kuchpwa
xiv. maombi yawasilishwe kwa anuani ifuatayo 

MKURUGENZI MTENDAJI (W),
S.L.P 1288,
KISHAPU. 

masharti yalioko kwenye tangazo hili yasomwe kwa makini na yazingatiwe
Share This
Previous Post
Next Post

FURSA AJIRA Is is an East Africa site which announcing, publishing job vacancies everyday from the government portals, recruiters agencies, organizations, companies and institutions to those jobless people. Get your dream job by visiting this site everyday or just install Fursa Ajira App

0 comments: